top of page

CHINA YAITEKA BOTI YA UVUVI YA TAIWAN Na VENANCE JOHN

Kikosi cha walinzi wa Pwani cha China hapo jana Julai 3 kimeiteka meli ya uvuvi ya Taiwan na kuwapeleka watu watano waliokuwa kwenye meli hiyo katika bandari iliyopo pwani ya China bara. Boti hiyo ya uvuvi kwa jina la Ta Chin-te Man 88 ilikuwa eneo la kiasi maili 27 kaskazini mashariki mwa Kinmen eneo ambalo liko chini ya himaya ya kisiwa cha Taiwan karibu na Pwani ya China.

Uongozi wa walinzi wa pwani ya Taiwan umesema kuwa kikosi cha ulinzi wa Pwani cha Taiwan kilijaribu kwenda kutoa msaada kwa wenzao baada ya kuwekwa chini ya ulinzi na wanamaji wa



China lakini walizuiliwa na kikosi cha China.

Hali katika kisiwa cha Taiwan, kisiwa ambacho kinajitawala lakini  China ikidai kuwa ni miliki yake imekuwa kwa siku za karibuni ya kutishia kuzuka kwa vita kati ya Taiwan na China hasa baada ya kisiwa cha Taiwan kumpata Rais mwenye msimamo mkali wa kuitaka China kutoingilia masuala ya ndani ya Taiwan.

Taiwan imeitaka China kuachilia meli hiyo na watu hao, wawili wa Taiwan na watatu wa Indonesia, ambayo inashikiliwa huko Weitou, bandari ya kusini-mashariki.

"Meli ya wavuvi ilikiuka kanuni za kusitisha uvuvi na ilitembea kinyume cha sheria ndani ya eneo lililopigwa marufuku," Liu Dejun, msemaji wa Walinzi wa Pwani ya China, amesema.

Msemaji huyo pia ameishutumu Taiwan kwa kutumia zana zisizo sahihi za uvuvi hivyo kuharibu rasilimali za baharini. Mpaka sasa Taiwan bado haijajibu lolote kuhusu madai hayo ya China.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page