top of page

CHINA YAMHUKUMU KIFO MWANAUME KWA KUWASHAMBULIA WAJAPAN BAADA YA MTU HUYO KUPOTEZA KAZI

Na VENANCE JOHN


Mwanaume mmoja wa China aliyemshambulia mama na mtoto wa Japan kwa kisu na kumuua mwanamke wa China aliyejaribu kuwalinda amehukumiwa kifo. Taarifa hii imetolewa na serikali ya Japan. Shambulio hilo lilifanyika nje ya shule ya Japan katika jimbo la China la Suzhou na lilikuwa moja ya mashambulizi matatu dhidi ya wageni nchini China mwaka jana.


Mahakama ya China imesema kuwa mwanaume kwa jina la Zhou Jiasheng, mwenye miaka 52, alitekeleza shambulio hilo tarehe 24 Juni baada ya kupoteza matumaini ya kuishi, kufuatia kupoteza kazi yake na kusongwa na madeni.


Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri Yoshimasa Hayashi aliwaambia waandishi wa habari kwamba mahakama iliamua kwamba shambulio hilo lilikuwa mauaji ya kukusudia na adhabu ilitolewa kutokana na athari kubwa kwa kijamii ambayo uhalifu ulitokea.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page