top of page

CHINA YAWANYONGA MADEREVA WALIYOWAUA MAKUMI YA WATU KWA GARI, MMOJA ALIFANYA HIVYO SABABU YA TALAKA

Na VENANCE JOHN


China imewanyonga wanaume wawili madereva waliohusika na mashambulizi mawili mabaya ndani ya wiki moja mwezi Novemba mwaka jana. Fan Weiqiu, mwenye umri wa miaka 62, aliwaua takribani watu 35 na kujeruhi makumi ya wengine baada ya kutembeza gari lake ndani ya watu wanaofanya mazoezi nje ya uwanja wa michezo wa Zhuhai.


Shambulio hilo linadhaniwa kuwa baya zaidi katika ardhi ya China kwa muongo mmoja. Siku kadhaa baadaye, Xu Jiajin, mwenye umri wa miaka 21, aliwaua watu wanane na kuwajeruhi wengine 17 katika tukio la kuwachoma visu katika chuo kikuu chake katika mji wa mashariki wa Wuxi.


Mamlaka zimesema kuwa Fan Weiqiu alisukumwa na kutoridhika kuhusu jinsi mali yake ilivyogawanywa kufuatia talaka yake na ndiyo akaamua kutekeleza tukio hilo. Huku ikielezwa kuwa Xu Jiajin alitekeleza shambulio lake baada ya kushindwa kupata diploma yake kutokana na matokeo mabaya ya mitihani.


Mwezi Desemba, Fan Weiqiu alipatikana na hatia ya kuhatarisha usalama wa umma, na mahakama ikielezea nia yake kama mbaya sana na mbinu zilizotumiwa za ukatili. Kunyongwa kwake siku ya leo kunakuja chini ya mwezi mmoja baada ya mahakama kumhukumu kifo.


Katika kesi ya Xu Jiajin, polisi walisema alikiri uhalifu wake bila kusita tarehe 16 Novemba na alihukumiwa kifo tarehe 17 Disemba, huku mahakama ikisikiliza kwamba mazingira ya uhalifu wake yalikuwa mabaya sana.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page