
Muziki unalipa ila juhudi na ubunifu uwepo wa kutosha ongeza na Bahati pale Mungu anapoamua iwe na itakuwa ambapo mfano halisi ni msanii Chino Wanaman kwani milango inazidi kufunguka kwake kila siku.
Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram amepakia picha hizi akiwa kwenye gari zake mbili mpya aina ya Jeep na BMW nakuandika "I Love My Cars" hii ni ishara tosha namna gani anafurahia matunda ya kazi yake, hii ikawe chachu ya mapambano kwako pia mdau ambaye unapambana na unatamani siku moja ndoto zako zitimie ili ufanye mambo makubwa nasi Msasa Media tunasema kila jambo linawezekana ni suala la muda tu kikubwa usikate tamaa.
Commentaires