Na VENANCE JOHN
Rais wa Colombia Gustavo Petro amezipiga marufuku ndege za kijeshi za Marekani ambazo zilikuwa zimebeba wahamiaji waliofukuzwa kuingia kuingia nchini Colombia. Haya yanajiri baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuanza kutoza ushuru wa 25% kwa bidhaa za Colombia.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_9c5782f430cc4719b4d521a21035926f~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_9c5782f430cc4719b4d521a21035926f~mv2.jpeg)
Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataiwekea Colombia ushuru wa asilimia 25 na vikwazo baada ya rais wake kuzuia ndege mbili za kijeshi za Marekani zilizokuwa zimebeba wahamiaji waliofukuzwa nchini Marekani.
Trump amesema ushuru wa bidhaa zote zinazoingia Marekani kutoka Colombia utawekwa mara moja, na katika wiki moja ushuru wa 25% utapandishwa hadi 50%. Rais wa Colombia Gustavo Petro alijibu kwa kusema atatoza ushuru wa kulipiza kisasi wa 25% kwa Marekani.
Mapema siku ya jana Jumapili, Rais wa Colombia Gustavo Petro alisema amekataa kuingia katika ndege za kijeshi za Marekani na kwamba atawapokea raia wa Colombia waliofukuzwa nchini Marekani, bila kuwachukulia kama wahalifu na ikiwa watarejeshwa kwa ndege za kiraia.
Comments