top of page

DADA WA KAZI AINOGESHA VIDEOYA NANDY NA BILLNASS "TOTORIMI"

Mapema hii leo Nandy aliwastua mashabiki zake baada ya kupost picha ya Dada wa kazi na kuweka maneno yasemayo "Sikutegemea kama unaweza kufanya hivyo Memo, Daaah" kauli iliyozua taharuki kwa mashabiki na kujiuliza nini kimetokea huku akikausha kimya bila kusema lolote.


Sasa Bhana jibu ni kwamba Kumbe mwanadada huyo amemtumia Dada wa kazi kama muigizaji ndani ya video ya wimbo wake wa Totorimi akiwa na Billnass ambapo Dada huyo kainogesha kweli kweli hivyo ilikuwa ni kiki tu ya kuweka sawa mashabiki kupokea kazi hiyo ambapo Nandy ameandika


"Dear MEMO umekua ndugu sasa siku napanga na @director_kenny kuusu video ya totorimi ulikuwa unamlisha NAYA pembeni ukaniambia dada mbona najua kuigiza nitumie mimi hutoamini na kweli sijaaaamini! Asante kwa kunipa video bora na nzuri..... kiukweli tulicho igiza humo ndani watu watuambie ndo wanayo pitia na wadada wao? maaana MEMO wangu walaaaaaaa kashavuka huko..."

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page