top of page
Radio on air

DAWASA YAANZA USAJILI MAGARI YA MAJISAFI DAR NA PWANI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza rasmi zoezi la siku saba la usajili, uhakiki na utoaji vibali vya uendeshaji wa huduma ya magari binafsi ya usambazaji Majisafi katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kwa lengo la kulinda



afya na usalama wa watumiaji wa huduma hiyo.

Zoezi hilo linafanyika katika maeneo ya Mbezi Makonde, Wazo, Mbezi Kibanda cha Mkaa, Mapinga, Kibaha, Mlandizi na Chalinze kwa lengo la kuwatambua na kuwapa vibali vya kutoa huduma ya Maji kwa njia ya Magari kwa Wananchi ambao hawana huduma au miundombinu ya Majisafi ya Mamlaka.

DAWASA inawahimiza Wananchi kutumia magari ya Majisafi yaliyopata uthibitisho kwa kuwekewa stika maalum zinazowaruhusu kusambaza huduma ya Maji ndani ya eneo lake la kihuduma.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page