top of page

DENMARK YAOMBA KUINUNUA CALIFORNIA YA MAREKANI, MAELFU WAVUTIWA NA KUTIA SAHIHI

Na VENANCE OHN


Waraka (petition) wa kejeli unaolenga kukusanya zaidi ya dola trilioni moja ili kuruhusu Denmark kuinunua California ya Marekani umepokea sahihi zaidi ya laki mbili (200,000). “Je, umewahi kutazama ramani na kuwaza, ‘Unajua Denmark inahitaji nini? Mwangaza wa jua zaidi, mitende, na viatu vya kuteleza kwenye barafu.’ Naam, tunayo fursa ya mara moja katika maisha ya kufanya ndoto hiyo kuwa kweli,” waraka huo unasomeka.


"Hebu tununue California kutoka kwa Donald Trump! Ndio, umesikia hivyo. California inaweza kuwa yetu, na tunahitaji usaidizi wako ili jambo hilo lifanyike. Ombi hilo linakuja baada ya rais wa Marekani kuonyesha nia mpya ya kudhibiti kisiwa cha Greenland, eneo lenye uhuru wake wa ndani lakini chini ya Denmark.


Waraka huo unaweka wazi sababu kadhaa kwa nini Denmark ingenufaika kutokana na ununuzi wa California, ikijumuisha uboreshaji wa hali ya hewa, usambazaji salama wa parachichi na utawala bora wa kiteknolojia. Trump, tangu kurejea madarakani kwa mara ya pili ameelezea udhibiti wa Marekani kwa Greenland kama lazima kabisa.


Maafisa katika Greenland na Denmark wamejitokeza kupinga vikali hamu ya Trump ya kupata kisiwa hicho ingawa maafisa wengi wa Denmark wanahofia kuwa Trump sasa yuko makini zaidi kuhusu wazo hilo kuliko wakati ilipokuwa katika muhula wake wa kwanza.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page