top of page

DEREVA ALIYESAMBAZA SAUTI KWENYE MITANDAO KUWA AMEJERUHIWA ENEO LA CHALINZE AKAMATWA, YABAINIKA YEYE NDIO MTUHUMIWA WA KUJERUHI

Taarifa kutoka jeshi la Polisi inaeleza kuwa


Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu sauti inayo sambaa kwenye mitandao mbalimbali ya Kijamii ikimhusu dereva anayeitwa Martin Gatolano miaka 42 Raia wa Nchini Rwanda akiomba msaada kwa madai ya kuchomwa kisu huko eneo la Chalinze.


Awali, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani tarehe 31/1/2025 majira ya saa 1:00 asubuhi ilipokelewa taarifa ya kuonekana kwa mwili wa mwanamke ukiwa pembezoni mwa Barabara ya Dar es Salaam Morogoro eneo la Chamakweza, Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani, akiwa hajitambui na mtupu pasipo kuwa na nguo yoyote mwilini, huku akiwa na jeraha kubwa linalodhaniwa kusababishwa na kukandamizwa na kitu butu kilichopelekea mguu kukatika kwenye goti huku mkono wa kushoto ukiwa umevunjika.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lilimchukua mtu huyo na kumfikisha Hospitali ya Wilaya ya Chalinze ambapo baada ya kupata matibabu ya awali, alijitambulisha kwa jina la Zakia Ibrahim miaka 40, mkazi wa Mlandizi na aliweza kueleza tukio zima lililompata na kupelekea majeraha kwenye mwili wake.


Uchunguzi wa awali umebaini dereva huyo alimpakia kwenye gari Zakia Ibrahim maeneo ya Ruvu Darajani majira ya saa 10:00 alfajir lenye namba za usajiri RAG 924E Lori aina ya Benzi na kwa mujibu wa GPS ya gari hilo na maelezo ya Zakia Ibrahim, imebainika kuwa gari hilo lilisimama zaidi ya dakika 15 na wawili hao wakiwa wamekubaliana kufanya mapenzi. Baada ya kitendo hicho kulitokea vurugu za kutokuelewana baina yao, na kupelekea ugomvi na dereva huyo alimsukuma nje dada aliyekuwa nae ndani ya gari aitwaye Zakia Ibrahim na kudondoka chini kisha kuvunjika mkono wa kushoto. Wakati dada huyo akiwa bado yupo chini, dereva huyo Martin Gatolano aliwasha gari kisha kumkanyaga mguu wa kushoto kwenye goti na kusagika.


Aidha, dereva huyu aliendesha gari mpaka eneo la Halmashauri ya Chalinze umbali wa Kilomita 15 toka eneo alilofanya tukio na kupaki gari pembeni katika sauti iliyorekodiwa kama inavyosikika ikilalamika kuwa amechomwa kisu na mtu aliyempa lifti na na kumsababishia jeraha kwenye paja la mguu wa kulia.


Hivyo, tunapenda kuwahabarisha umma ya kuwa, taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya Kijamii kuhusu dereva huyo kuchomwa kisu ni ya upotoshaji na siyo ya kweli. Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, liamshikilia dereva wa lori hilo kwa mahojiano zaidi kufuatia tukio hilo na uchunguzi ukikamilika atafikishwa kwenye vyombo vingine vya kisheria kwa hatua zaidi.


Kadhalika, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa rai kwa Jamii kuacha kueneza taarifa kwenye mitandao ya kijamii zisizokuwa na ukweli (uongo) na kusababisha taharuki. Pia halitasita kuwachukulia hatua kali wale wanaoeneza taarifa kwenye mitandao ya kijamii za upotoshaji na kuchafua taswira ya Mkoa wa Pwani kiusalama.

Comments

Couldn’t Load Comments
It looks like there was a technical problem. Try reconnecting or refreshing the page.
Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page