Ni furaha iliyoje pale yule aliyekutangulia katika jambo fulani maishani akapendezwa na kile unachokifanya.

Hichi ndicho kilichomkuta msanii wa kizazi kipya @officialbexytz anayefanya vyema na kazi yake mpya ya #MunguBaba ambapo staa wa Bongo Fleva @DiamondPlatnumz ameonekana kuvutiwa na kazi hiyo kiasi cha kutia like kwenye Instagram ya msanii huyo.
Bexy ameeleza kufurahishwa na jambo hilo na kusema Simba amekuwa mtu wa kusapoti vijana wenzake wenye vipajii hivyo ni faraja kwake kuona staa huyo ametembelea ukurasa wake wa Instagram na kupenda kile anachokifanya.
Ngoma hiyo tayari inapatikana kwenye platform mbalimbali za muziki ikiwemo YouTube ambapo unaweza kuicheki kupitia link hii
Comments