Staa wa Bongofleva Diamond Platnumz ametangaza burudani ya kukata na shoka kwa wakazi wa Dar es Salaam ikiwa ni kitambo toka afanye shoo kubwa jijini humo sasa ameona akate kiu ya mashabiki zake.
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya Ujio wa Tamasha kubwa la #BiteVibes chini ya
![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_efcf9a11d6774a76a009a6e19496a3cc~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_efcf9a11d6774a76a009a6e19496a3cc~mv2.jpg)
Serengeti Premium Lite Diamond amesema
"@serengetipremiumlite walivyosikia tunataka kukutana na Watanzania na Kusheherekea Utanzania Wao Moja kwa Moja Wakawa Onboard. Kwasababu Serengeti ni Bia ya Watanzania Kujivunia Utanzania Wao, Boss amesema Tamasha la #Hadhi YaJuu (Bite Vibes) Pale Viwanja vya Posta Kijitonyama kiingilio kiwe Bia ya Serengeti Tu" @diamondplatnumz
Kwa upande wake Ester Raphael ambaye ni Meneja Chapa wa Serengeti breweries amesema
"Ni Siku Kubwa sana Kwetu @serengetipremiumlite kuwa hapa Leo na Kwa Mara ya Kwanza Tumeweza Kuungana na Msanii Mkubwa Sio Tu Tanzania, Afrika Mashariki Bali Afrika Nzima na Dunia kwa Ujumla"
Shoo hiyo itafanyika Aprili 26 na 27 katika viwanja vya Posta Kijitonyama ambapo orodha ya wasanii mbalimbali watakaotumbuiza itaanza kuwekwa hadharani pamoja na suprise nyingi zitaendelea kuwekwa wazi hadi katika kilele cha shoo hizo.
Comments