top of page
Radio on air

DIDAH ATOA ONYO WATU WANAOTUMA MESSAGEKWA MTOTO WAKE INSTA DM....

Mtangazaji wa Wasafi FM Didah wa kipindi cha MashamSham amefunguka na kuwataka watu



wanaozama DM kwenye ukurasa wa Instagram wa mtoto wake waache mara moja kwani yeye ndio anaendesha akaunti ya mwanae na anaona kila kitu ambapo amemwaga maneno akisema

"Nawaona wanaume mnaoanza kuja DM kwa mwanangu Samira huko Instagram, hata aibu hamna wengine wafanyabiashara maarufu na wacheza mpira mnakuja kumtongoza mwanangu mmuharibie maisha, kama mlikuwa hamjui simu yake ninayo mimi na account yake naiendesha mimi, sitaki mchezo na binti yangu, ana miaka 15 bado ni mdogo na ni mwanafunzi, kinachowawasha nini?" Alifunguka Didah

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page