top of page

DKT. BITEKO AIWAKILISHA TANZANIA UAPISHO RAIS MPYA WA BOTSWANANa VENANCE JOHN

Na VENANCE JOHN


Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati, Dkt. Doto Biteko ameiwakilisha serikali ya Tanzania katika sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Botswana Gideon Duma Boko zitakazofanyika leo katika uwanja wa taifa wa nchi hiyo


Akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Gaborone, Dkt. Biteko amepokelewa na katibu mkuu wa vijana, jinsia, utamaduni na michezo, Bridget John, balozi wa Tanzania nchini afrika kusini, Bw. James Bwana pamoja na maafisa wengine waandamizi wa nchi hiyo.


Gideon Duma Boko ni rais wa sita Botswana ambaye alishinda kupitia chama cha Umbrella for Democratic Change. Uchaguzi mkuu nchini Botswana ulihitimishwa tarehe 30 Oktoba, 2024 ambapo Rais Mteule Gideon Boko aliibuka mshindi.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page