top of page

DOGO ALIEAMUA KUSEPA KWAO KWENDA KUISHI KWENYE TRENI ANATUMIA MIL 22 KWA MWAKA...

Kutana na Kijana mmoja kutoka nchini Ujerumani aitwaye Lasse Stolley (17) anadaiwa kuhama kwa wazazi wake na kwenda kuishi katika treni za 'Deutsche Bahn' kwa mwaka mmoja na nusu sasa.




Stolley alihama kwa wazazi wake akiwa na miaka 16 hapo awali ilikuwa ni ngumu kwa wazazi kukubali lakini baadaye wazazi wake walikubali kumuunga mkono kwenda kuishi maisha yake ya pekee.

Inasemekana kuwa Lasse hutumia dola 9,000 ambayo ni zaidi ya Tsh milioni 22 kwa mwaka pesa ambayo anatumia kwa ajili ya kununua tiketi.

Kufuatiwa na mahojiano yake ya hivi karibuni ameeleza kuwa japo maisha ndani ya treni siyo ya faragha lakini ana-enjoy kuishi humo ambapo ameweka wazi kuwa usiku hulala kwenye treni inayotembea ya Intercity Express (#ICE) na wakati wa mchana anakaa kwenye viti na kufanya kazi kama mtayarishaji program.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page