Hatimaye Ligi Kuu ya NBC imetamatika hii leo katika michezo 8 iliyopigwa kutoka kwenye viwanja tofauti tofauti hivyo kwa msimamo uliopo
Klabu ya Yanga SC ndio mabingwa huku washindi wa pili ni Azam FC na hawa ndio watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.
Kwa upande wa nafasi ya tatu washindi ni Simba na nne ni Coastal Union ambapo hawa kwa
![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_38632ec68710453cbe77c96084574f6e~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_38632ec68710453cbe77c96084574f6e~mv2.jpg)
pamoja watacheza Kombe la Shirikisho Afrika CAFCC.
Aidha Play Off itakuwa ni kati ya JKT Tanzania na Tabora United FC kucheza play-off huku Geita Gold na Mtibwa wakishuka Daraja.
Aidha Mbio za Mfungaji Bora sasa zimefikia tamati huku Aziz Ki akiibuka Mfungaji bora kwa kuweka kambani mabao 21 ambapo mchezo huu wa mwisho ametupia mabao matatu (Hat- Trick) Yanga SC wakishinda 4 - 1 dhidi ya Prisons ambapo amemtupa chini Feisal Salum aliyemaliza msimu kwa mabao 19 akifunga bao moja kwenye mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold uliotamatika kwa 0 - 2.
Simba SC 2-0 JKT Tanzania
Coastal Union 0-0 KMC
Mashujaa FC 3-0 Dodoma Jiji
Ihefu SC 5-1 Mtibwa Sugar
Yanga SC 4-1 Prisons
Namungo FC 3-2Tabora United
Geita Gold 0-2 Azam FC
Singida FG 2-3 Kagera Sugar
Asante kwa kufatilia ukurasa wako wa Msasa Media hususani kwenye upande wa habari za michezo kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 tukutane msimu ujao wa 2024/25 panapo majaliwa.
Comments