Na VENANCE JOHN
Majengo mawili mpya ya urefu wa futi 591, yaliyounganishwa juu na bwawa angani, yanatazamiwa kujengwa huko Marasi Marina, Dubai. Lakini bwawa hilo litakuwa na futi 43 halitafikiwa na umma, au hata kwa wakaazi wengi watakao kuwa wanaishi kwenye mojawapo ya majumba hayo ya kifahari.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_59f4f4014a10405687b22f7d16ee5ea6~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_59f4f4014a10405687b22f7d16ee5ea6~mv2.jpeg)
Wasanifu wake wanaeleza kuwa hilo litakuwa ni jumba la kipekee. Ikijumuisha makazi 63 ya kifahari, majengo hayo yaliyopewa jina la Regent Residences Dubai yatakuwa na thamani ya takriban dola bilioni 1 yatakapokamilika mwaka wa 2027.
Majumba hayo yatakuwa na upenu wenye ukubwa wa futi za mraba 35,000, vyumba sita vya kulala, chumba cha mazoezi ya mwili na lifti ya kibinafsi. Vyumba vingine vya mradi, ambavyo vyote vina ukubwa wa zaidi ya futi za mraba 6,500, kila kimoja kitachukua sakafu nzima.
Na wakazi hawatakuwa na haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kukosa bwawa kwa kuwa vyumba vyote vitakuwa na mabwawa yao ya kibinafsi ya kuogelea. Kampuni ya mali isiyohamishika ya Sankari ndiyo iliyoanzisha mradi huo pamoja na IHG Hotels & Resorts.
コメント