top of page

DUBAI NIMEENDA MARA NYINGIKULIKO MOROGORO - BILLNASS

Kutoka kwa msanii Billnass amefunguka ujumbe huu wa hamasa kwa vijana wenzake akiwa na Mama yake huko Ulaya.


"Nikikumbuka niliwahi Kuwa na Ndoto ya Kwenda Africa Kusini...Hata kwa kuiba na Nikawasimulia rafiki zangu kua nitaenda South Africa...wakanicheka sana na kuniambia unadhani South Africa ni Majani Mapana au Kisosora!! Lakini Sikukata tamaa nilibahatika kwenda South nikiwa Bado Nasoma na nikaenda tena na tena na Nikaenda Dubai Mara ya Kwanza nikiwa Chuoni... Imefika Hatua South na Dubai nimeenda Mara Nyingi kuliko Mara nilizoenda Morogoro...Na Nimeweza Kwenda Mataifa Mengine Makubwa Mengi sio kufanya Show wala Kutafuta Maisha Bali Kutembea tu... pia nimeweza Kusafiri na Watu ni wapendao Karibu Kila Mwaka Mke Wangu na Mtoto Wangu...Na Nilitamani Sana kusafiri na Wazazi Wangu lakini maokoto yalikuwa Hayajakaa... Mungu ni Mwema Birthday ya Mama Mwaka Huu atasherekea Europe na Mungu ampe Maisha Marefu Next time Aje na Baba na Wajukuu zake...!! Lengo la Maneno Yote Haya ni Kukutia Moyo kijana Mwenzangu wa Mtaani...Usikate tamaa.... Yote yanawezekana ipo Siku utawapa Furaha unaowapenda na Utafurahia Maisha kama Unavyotamani...Kwa Mungu Hakuna Kinachoshindikana."

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page