top of page

ENOCK AKAMATWA NA WALINZI WAKANISA AKITOROKA NA SAKRAMENTI


Kutoka Ifakara mkoani Morogoro Kijana Enock George Masala (19) amekamatwa akitoroka na Sakramenti takatifu baada ya kukomunika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Andrea Jimbo Katoliki Ifakara. Kijana huyo amekamatwa na walinzi wa Kanisa Hilo wakati wa Misa ya kwanza Asubuhi ya Leo Julai 28, na kutangazwa Kanisani Kwa tukio la wizi wa Sakramenti aliyotaka kutoroka nayo.



Paroko wa Kanisa kuu la Mtakatifu Andrea Jimbo la Ifakara Padre Marcus Mirwatu amesema kumekuwa na wimbi la matukio ya watu wasio wakatoliki wanaongia Kanisani kukomunika Kisha kuondoka na Sakramenti kinyume na taratibu na miongozo ya Kanisa Hilo. Kiongozi huyo wa Kanisa amelaani vitendo hivyo na kuaziga wakisto kuwafichua watu hao, wanaokwenda kinyume na Imani ya Kanisa Hilo, huku akiwataka walinzi wa Kanisa kuendelea kumuhoji kijana huyo ili kufahamu sababu za kijana huyo kufanya tukio Hilo.


"Tunashindwa kuelewa watu Hawa wanatumwa na nani kufanya vitendo hivi, hatuelewi Wana malengo Gani Kwa Kanisa letu, Hivyo ninaomba kijana huyu aendelee kuhojiwa kwanini amefanya tukio Hilo" ameeleza Paroko Padre Mirwatu.


Aidha kijana huyo Enork Masala alipohojiwa na mwandishi alikiri kuwa yeye si Mkristo Mkatoliki, na kwamba alitenda tukio Hilo baada ya kuona Wakristo wengine wakipanga foleni na kupokea Sakramenti, hivyo hakujua kama ni kosa kuondoka nayo Kanisani hapo huku akiweka bayana kuwa hakuna taratibu zote za kikanisa anazozifahamu.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page