top of page

ESMA ANGEKUWA NA MTOTO WA KIUME MWENYE MIAKA 23 SASA ILA ALIFARIKI AKIWA NA MIAKA 7

Esma Khan ambaye ni dada mkubwa wa nyota wa muziki nchini Tanzania Diamond Platnumz, ameeleza kwa ujasiri kisa cha kufiwa na mtoto wake wa kwanza, Osman, aliyefariki akiwa na umri wa miaka saba.


Akiongea kwenye Live ya Instagram, Esma alifunguka kuhusu tukio hilo lenye uchungu ambalo halijawahi kusemwa kwa kiasi kikubwa, ambapo alifichua hisia kali alizokuwa nazo alipotazama mwanawe akiaga dunia hospitalini. Esma anasimulia jinsi mtoto wake alivyofariki huku akimtaja Osman kuwa mtoto mzuri na anayejali ambaye alifanana naye kwa sana.


"Ningekuwa na mtoto wa kiume mkubwa sana.. Sa hii angekuwa na miaka 23. Nilimpemda lakini Mungu alimpenda zaidi. Alikuwa mtoto wangu wa kwanza kabisa. Alikuwa anaitwa osman. Alikuwa ni mtoto mzuri sana. Alinifuatwa mi kila kitu. Alikuwa mweupe sana. Na sasa hivi ningekuwa nasuluhisha ugomvi wa wakwe zangu lakini kwa bahati mbaya."


Alipata ugonjwa wa sickle cell. Nilikuwa naenda clinic mara nyingi sana. Alikuwa anatumia dose ya kila siku. Basi alifariki Kairuki. Kuna siku aliumwa tukaenda hospitali tukalzawa wiki. Tukaambiwa ukinywa dawa maini yako yanaharibika. Kwa hivo maini yake yaliharibika, figo na akafariki. Alifariki namuona." Esma. Kama angekuwa hai mtoto huyo basi Esma angekuwa na watoto watatu wakiwemo hawa wawili wa kike.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page