Na VENANCE JOHN
Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebook na Instagram imesema Watengeneza Maudhui nchini Tanzanja wanaotumia mitandao hiyo wataanza kulipwa kuanzia mwezi huu (Agosti 2024) ikiwa ni baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Serikali ya Tanzania.
Pia, META imelishukuru jukwaa la JamiiForums kwani ndiyo waliofanikisha mazungumzo kati META na Mamlaka za kiserikali pamoja na juhudi za kuhakikisha wazalishaji wa maudhui wanaelewa na kufuata Sera na mazingira salama na endelevu ya mtandaoni
Ikumbukwe kuwa, Machi 9, 2024, JamiiForums iliandaa mkutano na wabunifu wa maudhui mtandaoni (Wanawake) ili kujadili changamoto wanazo kutananazo kwenye majukwaa ya kidijitali ikiwemo masuala ya malipo.
Credits: JamiiForums
留言