top of page

FAINALI YANGA NA AZAM YAPELEKWA ZANZIBAR..

Fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB (CRDB Bank Federation Cup) sasa itachezwa katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar badala ya Babati mkoani Manyara


Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya baadhi ya miundombinu muhimu mjini Babati kutokuwa tayari kwa ajili ya fainali hiyo pamoja na sababu za kiusalama.

TFF imezishauri Mamlaka za mkoani Manyara kuendelea kufanya marekebisho katika miundombinu hiyo ili ifikiriwe kwa ajili ya fainali zijazo na michuano mingine mikubwa.

Fainali hiyo kati ya Azam FC na Yanga SC itachezwa Juni 2 mwaka huu katika Uwanja wa New Amaan kuanzia saa 2.15 usiku. TFF imemwalika Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita kuwa mgeni rasmi.

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page