top of page

FROLA MAPOLU WA GEITA AJIFUNGUA MAPACHA AMUUA MMOJA KUEPUKA USUMBUFU

Kutoka mkoani Geita Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia Flora Mapolu (33) mkazi wa kitongoji cha Mlima Namba 05 kata ya Lwamugasa wilayani Geita kwa tuhuma za mauaji ya mwanaye mwenye umri wa miezi miwili. Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, SACP Safia Jongo amethibitisha taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mjini Geita na kueleza mtoto huyo alikuwa mmoja ya watoto mapacha wa mama huyo.




Amesema Flora anatuhumiwa kutenda tukio hilo Julai 22, 2024 akiwa kitongoji cha Miyenze wilayani Bukombe ambapo akiwa na watoto wote anadaiwa kumnyonga mtoto mmoja kupunguza usumbufu.


"Julai 24 2024, jeshi la Polisi lilipata taarifa za uwepo wa mwili wa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi miwili ambaye aliuwawa kwa kunyongwa shingo na kisha kukatwa viungo vyake."


Kamanda amesema baada ya kufika eneo la tukio maofisa wa polisi walikuta mwili huo umekatwa mkono wa kulia na mguu wa kulia na kisha mwili wake kutelekezwa njia inayopitia shambani kwenda kisimani.


Source: HabariLeo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page