![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_42e2c359e51f437aa18fd8360d75b14c~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_42e2c359e51f437aa18fd8360d75b14c~mv2.jpeg)
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Goodluck Gozbert, amezua gumzo baada ya kuchoma moto gari alilopewa na Nabii GeorDevavie ambapo amesema sababu za kulichoma ni kwamba anaona gari hilo lilikuwa na uhusiano na madhabahu yasiyo sahihi, jambo lililomfanya aone ni muhimu kulitokomeza ili kulinda imani yake ya Kiroho.
Hatua yake imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakisifu ujasiri wake wa kulinda imani yake, wakati baadhi wakiona kama kitendo hicho hakikuwa na msingi. Tukio hili limefungua mjadala mpana kuhusu zawadi zinazopokelewa na watu kutoka kwa viongozi wa dini na umuhimu wa kuchunguza chanzo chake kabla ya kukubali. Goodluck ameongeza kuwa akipata kibali basi ataeleza zaidi juu ya hatua hiyo aliyochukua ya kuchoma gari hilo.
Comments