top of page

GRÍMSEY: KISIWA CHA CHENYE WATU 20 PEKEE NA NDEGE MILIONI 1, HAKUNA DAKTARI WALA POLISI

Na VENANCE JOHN


Ni kisiwa chenye ndege wengi, na wanyama kama punda, farasi na wengineo wengi kuliko idadi wa binadamu wanaoishi humo na kufanya shughuli zao. Grímsey ni kisiwa chenye ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 6.5 ambacho kiko umbali wa kilomita 40 kutoka pwani ya kaskazini ya taifa la Iceland.


Hadi mwaka wa 1931, njia pekee ya kufika kisiwa cha Grímsey ilikuwa kwa kutumia mashua ndogo iliyopeleka barua mara mbili kwa mwaka kwenye kisiwa hicho lakini siku hizi, safari za ndege za dakika 20 kutoka mji wa Akureyri na feri za saa tatu kutoka kijiji cha Dalvík hupeleka watu hadi kisiwa hicho cha miamba, ambao wengi wao, wanapenda kuona mojawapo ya aina za ajabu za ndege wa baharini na wanyamapori na makazi yao.


Inakadiriwa kuwa ndege wa baharini hapa ni wengi kuliko wakazi wanaoishi katika kisiwa cha Grímsey. "Huwezi kuamini, lakini ni watu 20 tu kati yetu wanaoishi hapa kwa muda wote," anaelezea Halla Ingolfsdottir, kiongozi wa watalii wa ndani na mmiliki wa Artic Trip.


Ingolfsdottir anasema "watu wanafikiri nilihamia hapa kwa ajili ya mapenzi, lakini nilipenda kisiwa hicho," anaeleza na kuongeza "kuna miujiza, na nilipenda jinsi watu walivyoishi hapa, wakazi wa kisiwa na asili. Hali ina nguvu sana hapa; ni nguvu tofauti ya asili wakati wa baridi, na pamoja na giza huja Nuru ya Kaskazini, nyota na dhoruba. Wakati wa masika huja mwanga, na ndege kila msimu ni maalum".


Katika kisiwa hicho hakuna hospitali, daktari au kituo cha polisi. Ikiwa katika kisiwa hicho cha Grímsey kutatokea dharura, Ingolfsdottir anasema kwamba walinzi wa Pwani na huduma za dharura wamewafunza wakazi wa kisiwa kuchukua hatua.


"Unapoishi hapa, lazima ujifunze kubadilika na kuzoea hali tofauti," Ingolfsdottir anasema. "Tumejitayarisha kwa lolote. Ikitokea dharura, wanatufundisha kuwa tayari kwa jibu la kwanza, na daktari huja kututembelea kila baada ya wiki tatu kwa ndege."

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page