top of page

GUINEA YAVUNJA VYAMA 67 VYA UPINZANI, NA KUBAKISHA VIWILI TU

Na Ester Madeghe,


Mamlaka ya Guinea imefuta na kuvunja makumi ya vyama vya siasa na kuacha viwili vikuu vya upinzani chini ya uangalizi, wakati ambapo serikali hiyo ya mpito ikiwa inajiandaa na uchaguzi.


Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekuwa ikiongozwa na utawala wa kijeshi tangu wanajeshi walipomwondoa madarakani Rais Alpha Conde mwaka 2021. Jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi inayojulikana kwa jina la ECOWAS imeshinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia na uchaguzi, ambao umepangwa kufanyika 2025.


Kuvunjwa kwa vyama 53 vya siasa na kuwekwa kwa vyama vingine 54 chini ya uangalizi wa miezi mitatu ni jambo ambalo halijawahi kutokea nchini Guinea, nchi ambayo ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 2010 baada ya miongo kadhaa ya utawala wa kimabavu.


Wizara ya Utawala wa Wilaya na Ugatuaji ilitangaza hatua hizo kulingana na tathmini ya vyama vyote vya kisiasa iliyoanza Juni. Tathmini hiyo ilikusudiwa "kusafisha hali ya kisiasa". Vyama 67 ambavyo vitakuwa chini ya uangalizi kwa miezi mitatu vinaweza kufanya kazi kama kawaida lakini lazima kutatua hitilafu zilizobainishwa katika ripoti.


Mamlaka imesema vyama vilivyowekwa chini ya uangalizi vimeshindwa kufanya kongamano lao la chama ndani ya muda uliopangwa, kutoa taarifa za benki, pamoja na masuala mengine. Guinea ni miongoni mwa nchi zinazokua za Afrika Magharibi zikiwemo Mali, Niger na Burkina Faso ambako jeshi limechukua madaraka na kuchelewesha kurejea katika utawala wa kiraia.

Kommentare


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page