top of page
Radio on air

HAILIE BINTI YAKE EMINEM AOLEWA KWA SHANGWE BAADA YA KUKAA MIAKA 8 KWENYE UCHUMBA NA MPENZI WAKE......

Imeibuka mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii baada ya binti wa msanii maarufu wa muziki kwa jina la Eminem, Kufunga ndoa ya heshima. Unaambiwa 50 Cent, Dk. Dre na Jimmy


Iovine walikuwa miongoni mwa wageni walioalikwa kwenye harusi ya Hailie Jade Scott na hilo lilionesha kufulika kwa nyota wengi zaidi kuliko wengi walivyodhani hapo mwanzo.

Eminem alivunja kabati lake na kuvaa suti ya tuxedo ikiwa ni ishara ya heshima kwa binti yake aliekua akiolewa. Mtoto wa pili wa rapa huyo, Hailie Jade Scott, alifunga ndoa na mchumba wake Evan McClintock Jumamosi huko Battle Creek huku sherehe yao ikiwa imehudhuriwa na marafiki wa karibu pamoja na familia.

Hakika ni mwanzo mwema wa hatua nyingine ya maisha yao kwa Hailie na Evan ambao wamekuwa pamoja kama wapenzi tangu 2016 na ambao walichumbiana Februari ya mwaka jana.Hailie ambaye ana umri wa miaka 28 sasa, ambaye ni mtangazaji na mshawishi wa mitandao ya kijamii, amekuwa mboni ya jicho la Eminem kwa miaka mingi baada ya kutajwa jina lake mara kadhaa katika nyimbo zake, huku Slim (Eminem) akifahamisha umma kuwa yeye ni baba mwenye kumlinda mwanae na ambaye angefanya chochote kwa ajili yake.

Usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari zaidi tembelea tovuti yetu www.msasamedia.com

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page