top of page

HALMASHAURI YA WILAYA YA NAMTUMBO YAVUKA LENGO UKUSANYAJI WA MAPATO

Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma imevuka lengo la ukusanyaji mapato,baada ya kufanikiwa kukusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 2.03 sawa na asilimia 101 katika kipindi cha mwaka 2024/2025.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Namtumbo Ndg. Philemon Mwita Magesa @philemonmagesa kwenye kikao cha Baraza la madiwani la kujadili taarifa za utekelezaji wa Shughuli za kamati za Kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Hesabu za Robo ya pili za Halmashauri kwa mwaka wa fedha za 2024/2025. Kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri hiyo.


Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Ndg. Haruna Mang’uli amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri wa Mapato. Mang’uli amewakumbusha wananchi wa Namtumbo kuhakikisha wanawapeleka watoto wao walio chaguliwa kujiunga masomo ya kidato cha kwanza kwenye shule walizopangiwa.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Juma Pandu amewapongeza watumishi na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato hali iliyosababisha kuvuka malengo ya makusanyo kwa asilimia zaidi ya 101.

Comentários


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page