Na VENANCE JOHN
Msemaji mkuu wa Hamas Sami Abu Zuhri anasema kuwa Rais wa Marekani Doanald Trump lazima akumbuke kwamba kuna makubaliano ambayo lazima yaheshimiwe na pande zote mbili ikiwa anataka mateka wa Israel warejeshwe.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_2b599eb26c9d40a3a94ad52186d53f1e~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_2b599eb26c9d40a3a94ad52186d53f1e~mv2.jpeg)
Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Sami Abu Zuhri amesema kuwa lugha ya vitisho haina maana na inatatiza mambo.
Ikumbukwe kuwa hapo jana, Trump aliwaambia waandishi habari kwamba mambo yatakuwa mabaya ikiwa mateka wote waliosalia wa Israeli hawataachiliwa na Hamas mwishoni mwa wiki hii. Mpaka sasa mateka 16 wa Israeli wameachiliwa ikiwa ni sehemu yakutekeleza mpango wa kusitisha mapigano, huku wakisalia 17. Kati ya hao 17, Israel inasema wanane tayari wamekufa.
コメント