top of page

HAPATOSHI DERBY YA KARIAKOO HAPA BARAKA MPENJA KULE GHARIB MZINGA KWENYE KIPAZA...

Ikiwa zimesalia siku mbili tu #DerbyYaKariakoo iweze kuwaka moto mambo yanazidi kutaradadi kwa kwenye kipaza cha Azam TV watakaounguruma nii #SautiYaRadi Baraka Mpenja na #Kilwa Finest Gharib Mzinga.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa watangazaji hao kutangaza kwa pamoja ambapo pia Mpenja itakuwa ni Derby yake ya 14 kutangaza huku Mzinga ikiwa ni ya pili toka aingie Azam



TV.

Mpenja amefunguka haya baada ya kupangwa na Gharib Mzinga kwenye kutangaza mchezo huo mkubwa kabisa Afrika Mashariki na Kati.

Mara zote inavutia kufanya kazi na mtu bora Sikuiona hii ikija kwa wakati huu, lakini Mungu ameamua iwe hivyo na Menejimenti yetu ya Azam Media LTD, imeamua kwa mara ya kwanza kwenye Derby ya Kariakoo Yanga na Simba, Mwamba wa Umalila Baraka Mpenja asimame na Kilwa Finest Gharib Mzinga @gharib_mzinga23

Woow! ni jambo kubwa ambalo limenivutia sana kwa sababu MZINGA kwa sasa ni Mtangazaji bora mno wa kandanda nchini.

Kwangu mimi itakuwa Derby ya 14 ya YANGA VS SIMBA, ALHAMDULILLAH!, lakini kwa MZINGA itakuwa mechi yake ya pili ya YANGA NA SIMBA.

All the best kwako my young brother Gharib Mzinga."

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page