top of page

HARMONIZE AELEZA KILICHOTOKEA HADI KUTAKA KUPIGANA NGUMI NA MWAKINYO NDANI YA GYM...




Siku ya jana kuna video imesambaa mtandaoni ikimuonesha staa wa Bongo Fleva Harmonize akirushiana ngumi na Bondia Hassan Mwakinyo ndani ya ukumbi wa kufanyia mazoezi (GYM) jambo lililoacha maswali mengi juu ya nini kimetokea ambapo sasa ameamua kutoa ufafanuzi kupitia ukurasa wake wa Instagram

Nitangulize neno sorry kwa yeyote aliekutana na Video Ya mzozano na Hassani was Tanga !!! Binafsi Sikuwahi Fikiria Kwamba Yupo Serious Nilikuwa Namchukulia Kama Mtuu Wa Maneno tu mtandaoni Ila kwabahati Mbaya Sanaa Jana Wakati Naingia GYM kanitolea Maneno Ya dharau!! Na matusi Ya kuhusisha Hadi Mzazii !!! Nilishindwa Kujizuia!!! Kama mwanadam Pengine Ningeweza Kutumia Busara Zaidi!! Ila hasira Zilipelekea Utata huo!!!! Itoshe Kusema IPO HAJA YA KULINDA HESHIMA YANGU Sambamba na Kumuambia Asikalili watu!! MWAKINYO LETS MAKE IT OFFICIAL TWENDE ROUND 6 MTUU MBILI !! Ili tuheshimiane !!!" Ameandika Harmonize.

Comments

Couldn’t Load Comments
It looks like there was a technical problem. Try reconnecting or refreshing the page.
Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page