top of page

HATIMAYE RAIS RUTO ALIVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI KAMA GEN-Z WALIVYOHITAJI, ASEMA SERIKALI INAANZA KUPAMBANA NA UFISADI....

Na VENANCE JOHN

Rais William Ruto wa Kenya amelivunja baraza lake la mawaziri na kuziacha nafasi mbili pekee ya Kiongozi wa mawaziri na Waziri wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi na ofisi ya naibu wa rais Rigathi Gachagua .




Rais Ruto amesema atachukua muda kufanya majadiliano ya kuunda baraza jipya la mawaziri litakalohusika na uendeshaji wa serikali.

'Mara moja nitashiriki katika mashauriano ya kina katika sekta mbalimbali na miundo ya kisiasa, kwa lengo la kuunda serikali pana ambayo itanisaidia katika kuongeza kasi na kuharakisha yanayohitajika, ya haraka pamoja na utekelezaji wa mipango mikali ya kukabiliana na mzigo wa madeni, kuongeza rasilimali za ndani, kupanua nafasi za kazi, kuondoa uharibifu wa fedha na marudio yasiyo ya lazima ya msururu wa vyombo vya serikali na kuua joka la ufisadi hivyo kuifanya serikali kuwa isiyo na gharama kubwa , na yenye ufanisi". Amesema rais Ruto kupitia hotuba yake.

Rais Ruto amesema wakati akiendelea na mchakato wa kuliteua baraza jipya la mawaziri ,shughuli za serikali zitaendelea bila kuvurugwa chini ya uongozi wa Makatibu wakuu na maafisa wengine husika.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page