top of page

HII NDIO SABABU YA RAIS SAMIA KUTAKA SIMBA AITWE “TUNDU LISSU”, LISSU ATOA NENO

Na VENANCE JOHN


Bila shaka unakumbuka wanyama waliowahi kuvuma na kushika vichwa vya habari, wanyama waliokuwa wamepewa majina ya viongozi wakubwa ndani ya nchi. Wanyama kama Faru Magufuli, ⁠Faru Majaliwa, Faru Ummy Mwalimu, Faru Janet Magufuli, Faru Pius Msekwa, Faru Ndugai, Faru Obama, Faru Hillary Clinton, na Faru Samia ambaye yupo kwenye mchakato wa mwisho kupewa jina hilo.


Lakini mwishoni mwa wiki iliyopita, simba aliyepewa jina la Tundu Lissu ndiyo simba anayetamba sana kwenye mitandao ya kijamii.


Simba huyo amejizolea umaarufu ndani ya saa kadhaa baada ya rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutaka simba aliyekuwapo katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Unguja, visiwani Zanzibar kupewa jina la mwanasiasa maarufu ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Bw Tundu Lissu


Simba ‘Tundu Lissu’ ambaye kwa sasa ana miaka 7 alizaliwa Januari mosi, 2018, Dar es Salaam (Dar es salaam Zoo), nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam, eneo la Mwasonga katika Wilaya ya Kigamboni.


Simba huyu ana asili ya hifadhi mchanganyiko za mapori ya Akiba ya Grumeti na Ikorongo yanayopatikana katika mfumo wa ikolojia ya Serengeti, Kaskazini mwa Tanzania ambako ndiko wazazi wake walitokea kabla hawajahamishiwa Dar es Salaam Zoo. Hivyo samba “Tundu Lissu” unaweza kumwita mjanja wa mjini


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametaja sababu za kumpa simba jina hilo kuwa ni kutokana na umachachari na ukorofi wa mwanasiasa huyo.


“Nataka niseme kulikuwa kuna vijiclip vinarushwa kulikuwa kuna simba machachari pale mkorofi kidogo, nikauliza huyu simba mmempa jina? Nikaambiwa bado, nikawaambia muiteni Tundu Lissu kwa sababu alikuwa hatulii kama alivyo mwanangu Tundu Lissu," alisema Rais Samia.


Wakati Rais Samia akitaja sababu za kutaka simba aitwe jina la Tundu Lissu, Tundu Lissu mwenyewe amesema mkuu wa nchi yupo sahihi kutokana na asili ya ukoo wa Tundu Lissu. Lissu amesema Rais Samia yupo sahihi, kwani yeye amezaliwa kwenye ukoo wa mashujaa wa Kinyaturu, watu waliowahi kuua simba wanaokula ng'ombe na wezi wa ng'ombe wao.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page