top of page

HISPANIA KUWEKA USHURU WA 100% KWA NYUMBA ZA WAKAZI WASIO WA UMOJA WA ULAYA

Na VENANCE JOHN


Nchi ya Hispania inapanga kutoza ushuru wa hadi 100% kwa mali zinazonunuliwa na watu wasio wakaazi kutoka nchi zilizo nje ya Umoja wa Ulaya (EU). Akitangaza hatua hiyo, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Pedro Sánchez amesema hatua hiyo isiyokuwa ya kawaida ni muhimu ili kukabiliana na dharura ya makazi nchini humo.


Sánchez amesema hatua hiyo imeundwa ili kutoa kipaumbele kwa nyumba zilizopo ili kuwaduhumia wakaazi wa nchi hiyo kwanza kuliko kuwahudumia raia wa kutoa nchi nyingine hasa nje ya Umoja wa Ulaya wanaoingia Hispania kwa ajili ya utalii.


Sánchez hakutoa maelezo zaidi kuhusu jinsi kodi hiyo ingefanya kazi wala ratiba ya kuiwasilisha bungeni ili kuidhinishwa, ambapo mara nyingi amekuwa na shida kukusanya kura za kutosha kupitisha sheria. Lakini serikali yake imesema pendekezo hilo litakamilika baada ya utafiti makini.


Mojawapo ya hatua nyingi zilizopangwa zilizotangazwa na waziri mkuu zinazolenga kuboresha uwezo wa kumudu nyumba nchini humo ni pamoja na msamaha wa kodi kwa wamiliki wa nyumba wanaotoa nyumba za bei nafuu, kuhamisha zaidi ya nyumba 3,000 hadi kwa shirika jipya la makazi ya umma, na udhibiti mkali na ushuru wa juu kwa nyumba za watalii.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page