top of page

HIZI NDIZO BAA 50 BORA ZAIDI DUNIANI KWA 2024, AFRIKA HAINA MSHINDI KWENYE ORODHA HIYO

Na VENANCE JOHN


Jijini Madrid mjii mkuu wa Hispania, jana usiku kulifanyika hafla ya kutambua na kutoa tuzo kwa baa 50 bora zaidi duniani kwa mwaka 2024.


Kila mwaka maoni na uzoefu wa wataalam 700 wa tasnia ya baa kote ulimwenguni, hufanya maamuzi ya kuchagua baa bora zaidi na shirikisho hilo la baa 50 bora linasema hakuna vigezo maalum ambavyo majaji wanaombwa kuzingatia zaidi ya maoni yao binafsi.


Handshake Speakeasy ya Mexico City nchini Mexico imenyakua tuzo ya kuwa baa bora ulimwenguni. Haya ni mafanikio makubwa kwani baa hiyo ilifunguliwa mwaka jana na mwaka huo huo ilikuwa ya tatu lakini mwaka huu ndio imeongoza.


Baa iliyoshika nafasi ya pili ni Bar Leone ya mtindo wa Kiitaliano ya Hong Kong, China ambayo inalenga kueneza dhana ya "cocktail populari" ambayo kwa kiingereza ni "cocktail for the people," (cocktail kwa ajili ya watu) Nafasi ya tatu imeshikwa na iliyokuwa namba 1 mwaka jana, Sips ya Barcelona Hispania.


Baa zilizoongoza na kuingia kwenye 10 bora zaidi ni 1.Handshake Speakeasy, Mexico City, Mexico, 2.Bar Leone, Hong Kong, China 3.Sips, Barcelona, Hispania, 4.Tayer + Elementary, London, Uingereza, 5.Jigger & Pony, Singapore, 6.Line, Athens, Ugiriki, 7.Tres Monos, Buenos Aires, Argentina, 8.Alquimico, Cartagena, Colombia, 9.Zest, Seoul, Korea Kusini, 10.Paradiso, Barcelona, Hispania


Tuzo ya mhudumu wa baa, ambayo hutolewa kila mwaka kwa mtaalamu wa kutengeneza michanganyiko (mixologist) na hutolewa na wahudumu wenzake , ilitolewa kwa Iain McPherson ambaye baa yake imeshika nafasi ya 30 ya Panda & Sons ya Edinburgh, nchini Scotland.


Nafasi ya 50 imefungwa na baa kwa jina la 1930, Milan kutoka Italia. Katika orodha hiyo ya baa bora 50 zaidi duniani, kilicho washangaza wengi ni kwamba Afrika haijapata hata baa moja iliyoingia kwenye orodha hiyo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page