top of page

HOSPITALI YA SEKOUTOURE YAZINDUA HUDUMA YA UPASUAJI WA WAGONJWA WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure imezindua huduma ya Upasuaji wa tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi Machi 22, 2024.

Bi Claudia Kaluli Muuguzi Mkuu wa Mkoa akimuwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa amesema huduma hii ya Upasuaji wa Vichwa vikubwa na Mgongo wazi itaenda kupunguza wagonjwa ambao Kwa Kanda ya Ziwa walikuwa wanapata huduma hii katika Hospitali ya Bugando, sasa kuanz Kwa huduma hii itaenda kuboresha huduma Kwa Hospitali za Rufaa za Mikoa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Dr Bahati Msaki ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Kanda ya Bugando @bugandomedical Kwa kutuma wataalamu wa Upasuaji kuja Hospitali ya Sekoutoure na kuwapa Mafunzo Madaktari na



Wauguzi hii inaendelea kuboresha huduma.

"Pia niwaombe wananchi kutowaficha Watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi na kuwaleta hapa Hospitali ya Rufaa Kwa ajili ya kupatiwa huduma"

Huduma hii ilianza miezi mitatu iliyopita ikitolewa na Madaktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Bugando wakishiriana na Madaktari Bingwa na Wauguzi kutoka Hospitali ya Sekoutoure huku wagonjwa zaidi ya 20 wakifanyiwa Upasuaji na wanaendelea vizuri.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page