Na VENANCE JOHN
Shirika la Posta la Marekani limesema litasitisha kwa muda vifurushi kutoka China na Hong Kong, baada ya Rais Donald Trump kufunga mwanya wa biashara wiki hii unaotumiwa na wauzaji reja reja wakiwemo Temu na Shein kusafirisha vifurushi vya thamani ya chini bila kutozwa ushuru hadi Marekani.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_b49018ce96f346f089945ee53429e392~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_b49018ce96f346f089945ee53429e392~mv2.jpeg)
Utawala wa Trump uliweka ushuru wa ziada wa 10% kwa bidhaa za China, ushuru ambao ulianza kutumika hapo jana Jumanne. Mfumo wa awali ulikuwa unaruhusu waagizaji na wanunuzi wa Marekani kutolipa ushuru kwa vifurushi vyenye thamani ya chini ya dola 800.
Kampuni ya biashara ya mtindo ya Shein na duka la mtandaoni la Temu, ambao wote wanauza bidhaa kuanzia midoli hadi simu za kisasa, wamekua kwa kasi nchini China kutokana na msamaha wa ushuru kwa bidhaa za China nchini Marekani. Kampuni hizo mbili kwa pamoja zinaweza kuchangia zaidi ya 30% ya vifurushi vyote vilivyosafirishwa kwenda Marekani kila siku kwa mwaka 2023.
Comments