Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ametoa ufafanuzi juu ya video zilizosambazwa na Mange Kimambi akiwa na mwanamke mwingine ambapo amefunguka haya

"Nimeona Kuna clip zinasambazwa Mtandaoni zinazonihusu...Clip hizo ni za zamani, Mwaka 2023, na zina zaidi ya Miaka miwili nyuma... Na Mwanamke huyo pia niliachana nae takriban miaka Miwili sasa... Lakini pia nilimueleza Mwenzangu niliyenae na Tukasameheana na kuanza Maisha Mapya.
Mwanamke huyo sasa ameamua kutumia clip hizo na kuambatanisha na jumbe za Uongo kwa lengo la kuni blackmail na kutengeneza Fedha, jambo hili lishafikishwa katika Mamlaka Husika na Taratibu za Kisheria zinafuatwa. Shukrani" amefunguka Diamond kupitia Insta Story yake.
Komentáře