Na Ester Madeghe,
Utafiti wa hivi karibuni wa jarida la The Lancet unaonyesha kuwa idadi ya watu wazima wanaougua kisukari duniani kote imeongezeka zaidi katika miongo mitatu iliyopita, huku ongezeko kubwa ni katika nchi zinazoendelea.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_b2f6ea9202004a89b7bcb77c656734de~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_b2f6ea9202004a89b7bcb77c656734de~mv2.jpeg)
Utafiti huo unabainisha kwamba tatizo la kisukari limeathiri karibu asilimia 14 ya watu wazima duniani kote kufikia mwaka 2022, ikilinganishwa na asilimia saba mwaka wa 1990, ambapo zaidi ya watu milioni 800 duniani, wanaugua ugonjwa wa kisukari.
Watafiti wamesisitiza kuwa unene kupita kiasi ni sababu kubwa inayochangia watu wengi kuugua kisukari, huku pengo la kutibu ugonjwa huo baina ya nchi tajiri na maskini pia likiongezeka.
Mwandishi mkuu wa utafiti huo Majid Ezzati wa Chuo cha Imperial London amesema kuwa kukosekana kwa matibabu thabiti kunahatarisha matatizo mengine ya kiafya kwa watu wenye umri mdogo haswa katika nchi zenye kipato cha chini.
Comments