Mwigizaji Idris Sultan amewasili nchini Tanzania baada ya kukamilisha ziara ya mafunzo nchini
![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_81d2480076954d13978a97da5fde66ac~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_81d2480076954d13978a97da5fde66ac~mv2.jpg)
Korea Kusini ambapo mchana wa leo ametua Tanzania.
Ziara hii aliyoambatana na wasanii wengine wa filamu kama Steve Nyerere, Irene Uwoya, Irene Paul, Wema Sepetu, Getrude Mwita, Gabo, Dorah, Godliver Gordian, Eliud Samweli, Johari na Senator Msungu imezaa matunda baada ya timu nzima kupigwa Msasa na wataalamu wa filamu nchini Korea Ambapo pia walifanikiwa kufika Studio kubwa za Busan.
Tutarajie makubwa kwa Idris ambaye mara kadhaa ameshiriki kwenye filamu za Kimataifa ambazo zimepenya hata kwenye majukwaa makubwa ya kutazama maudhui ya Netflix na sasa macho ya wengi ni kuona wanayatimiza waliyojifunza huko.
Comments