Mwigizaji Idris Sultan akiwa kwenye ziara ya wiki moja nchini Korea Kusini, leo ikiwa ni siku ya pili mjini Seoul, amepata bahati ya kufanya kikao na Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Togolani Edriss Mavura ambapo walizungumza dhumuni la safari yao nchini humo ikiwa ni
![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_b435afd15e8144e68c30e9e1f3a10ee8~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_b435afd15e8144e68c30e9e1f3a10ee8~mv2.jpg)
kujifunza na kuongeza ujuzi kwenye tasnia waliyopo ili kukuza kazi zao Kitaifa na Kimataifa.
Idris ambaye pia ni mshindi wa Shindano la Big Brother Africa 2014 amekiri kushangazwa na Mhe. Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kutumiza ahadi ya kuwafungulia wasanii njia za kwenye kujifunza kwa vitendo kutoka mataifa yaliyoendelea kwenye uwekezaji hususani ndani ya tasnia ya sanaa kwani imekua haraka sana kwa wao kupata fursa hii ya kwenda kujifunza mambo makubwa yenye tija kwenye tasnia ya nzima ya filamu nchini Tanzania.
Hii ni fursa mpya kwa Idris ambaye tayari harakati zake za kufanya kimataifa zimefunguka kwani tayari ameshashiriki filamu za Kimataifa zilizompa nafasi ya kuonekana kwenye jukwaa kubwa la filamu duniani Netflix ambapo amefanya vyema kupitia filamu ya Slay na Married To Work.
Idriss ameongozana na mastaa wengine wa Bongo kama Irene Uwoya, Wema Sepetu, Steve Nyerere, Gabo, Irene Paul, Eliud, Stanley Msungu, Godliver Gordian, Dorah na Getrude Mwita.
コメント