top of page

IKIWA NI KILELE CHA WIKI YA LISHE KITAIFA NAMTUMBO WANUFAIKA NA ELIMU YA LISHE

Kutoka mkoani Ruvuma Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kupitia divisheni ya afya , ustawi wa jamii na lishe inaadhimisha Kilele cha wiki ya lishe kitaifa ikiwa na lengo la kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa jamii sambamba na kufuata mtindo bora wa maisha.


Akizungumza wakati akitoa elimu hiyo kwa wakazi wa mtaa Namtumbo uliopo kata ya Namtumbo Afisa lishe wa Halmashauri hiyo Bi.Neema Kivelia amewaeleza wakazi hao kuwa wanaweza kufanya kilimo cha mboga mboga na matunda kwa kutumia vitu mbalimbali vinavyoweza kuhifadhi udongo kwa kutengeneza bustani ndogo kulingana na ukubwa wa eneo na kupanda kwa mpangilio mzuri.


"...ni muhimu watu wote kupata lishe bora kwa kuzingatia makundi sita ya vyakula,eneo lako dogo linaweza kuwa na tija kubwa ikiwemo na kukupunguzia gharama kubwa za kununua mboga kila siku..." amesema Bi.Neema


Tekla Ndunguru ni Mwananchi wa Eneo la Mtaa wa Namtumbo mjini amewataka akina mama wajawazito na wanaojifungua kuhakikisha wanafuatilia afya zao kwa kula mlo kamili wenye virutubisho vyote kwa viwango sahihi.


Bi Neema ameongeza kuwa maradhi mengi yanaweza kuepukwa kwa kula vizuri na kufanya mazoezi na kuachana na mitindo ya maisha isiyofaa kama vile kuacha unywaji pombe uliokithiri na uvutaji wa sigara.


Aidha amewakumbusha kina mama kuzingatia ulaji mzuri ndani ya siku 1000 muhimu kuanzia mimba inapotungwa mpaka mtoto anapotimiza miaka miwili huku akikitaja kipindi hicho kuwa muhimu zaidi katika makuzi ya viungo vyote vya mwili wa mtoto sambamba na akili yake.


Commenti


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page