Na VENANCE JOHN
Msemaji wa serikali ya Iran Fatemeh Mohajerani ametangaza kuwa bajeti ya jeshi la nchi hiyo itaongezeka kwa 200%. Mapema wiki hii, wakati akiwasilisha bajeti yake ya kwanza kwa bunge la Iran, Rais Masoud Pezeshkian aliahidi kuongeza matumizi ya kijeshi, akitaja hali ya kikanda kama kisababishi cha kupelekea hali hiyo.

Ongezeko hilo la matumizi linakuja wakati wana mgambo wanaoungwa mkono na Iran katika eneo hilo, ambao kwa muda mrefu wanaonekana kama sehemu ya kuwafadhili, lakini kwa sasa wanadhoofishwa kwa kiasi kikubwa na mashambulio ya Israeli.
Kwa mara ya kwanza mwaka huu, Iran na Israel zilishambuliana moja kwa moja kwenye eneo la kila mmoja ambapo mwishoni mwa juma, Israel iliishambulia Iran , na kuua wanajeshi wanne na raia mmoja ikiwa ni kulipa kisasi cha shambulizi la Iran la Oktoba 1.
Comments