Na VENANCE JOHN
Hatimaye makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas yamefikiwa baada ya kushindwa kufikiwa mara kadhaa. Viongozi mbalimbali wa dunia wapongeza makubaliano hayo ya kusitisha mapigano Gaza na kuachiliwa kwa mateka ambayo yataanza kutekelezwa rasmi Jumapili mchana.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_8513ad865d9f4e9793b0146034baad92~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_8513ad865d9f4e9793b0146034baad92~mv2.jpeg)
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, ametoa wito wa kuwasilishwa kwa msaada wa haraka wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, akipongeza mpango uliofikiwa wa usitishwaji mapigano huko Gaza akisema umetokana na juhudi za Misri, Qatar na Marekani.
Wito kama huo umetolewa pia na viongozi mbalimbali wa ulimwengu ambao wamehimiza kuchukuliwa kwa hatua za ziada baada ya kufikiwa kwa makubaliano hayo wakisisitiza kuwapo kwa juhudi za kimataifa za kuyajenga upya maeneo yaliyoharibiwa na vita.
Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina, Mohammed Mustafa, amesema Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kuendelea kuishinikiza Israel kukubali kuundwa kwa dola huru la Wapalestina.
Kommentare