top of page

ISRAEL YAAPA KULIPA KISASI SHAMBULIO LILILOWAUA VIJANA NA WATOTO MILIMA YA GOLAN....Na VENANCE JOHN

Na VENANCE JOHN


Baraza la Usalama na vita la nchni Israel limeipatisha idhini kwa serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya kuamua hatua za kuchukua kujibu shambulizi la roketi lililosababisha vifo vya vijana na watoto 12. Shambulizi hilo lilitokea kwenye eneo lililonyakuliwa na linalokaliwa na Israel la milima ya Golan.




Israel na Marekani zinalilaumu kundi la Lebanon la Hezbollah kuhusika na hujuma hiyo ya siku ya Jumamosi lakini kundi hilo limekanusha madai hayo. Shambulizi hilo kwenye kitongoji cha Majdal Shams ndiyo shambulizi baya zaidi kutokea ndani ya Israel au katika maeneo yanayokaliwa tangu uvamizi wa kundi la Hamas wa Oktoba 7 mwaka jana, uliosababisha kuzuka kwa vita vya Gaza.


Israel imeapa kwamba itajibu shambulizi hilo dhidi ya Hezbollah na tayari jana Jumapili ndege za kivita za nchi hiyo ziliyapiga maeneo kadhaa ndani ya Lebanon.

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page