top of page

ISRAEL YASEMA IMEWAUA WAPIGANAJI WA HEZBOLLAH 250

Na VENANCE JOHN


Jeshi la Israel linakadiria kuwa limewaua takriban wapiganaji 250 wa Hezbollah, wakiwemo baadhi ya makamanda wa kikosi wa kundi hilo, tangu kuanza kwa operesheni yake ya ardhini nchini Lebanon mapema wiki hii.


Taarifa hii ni kwa mjibu wa msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari msemaji leo Ijumaa. Hii inaendelea kuonesha uhasama unaoendelea kati ya Hezbollah na wanajeshi wa Israel nchini Lebanon. Kwa sasa moshi unafuka katikati mwa kikongoji cha Tiro, kusini mwa Lebanon.


Luteni Kanali Nadav Shoshani amesema wanajeshi bado wanatathmini uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya anga kusini mwa Beirut, usiku wa jana, ambayo amesema yalilenga makao makuu ya kijasusi ya Hezbollah. Hata hivyo mpaka sasa kundi la Hezbollah halijatoa hadharani idadi yoyote ya vifo.

Commenti


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page