top of page

JACOB KIPLIMO MWANARIADHA WA UGANDA AVUNJA REKODI YA DUNIA YA MBIO ZA NUSU MARATHON

Na VENANCE JOHN


Mwanariadha wa Uganda Jacob Kiplimo amekuwa mtu wa kwanza kuvunja rekodi ya dakika 57 katika mbio za nusu-marathon. Jacob Kiplimo ameweka rekodi mpya ya dunia kwa kukimbia dakika 56 na sekunde 42 mjini Barcelona, nchini Hispania. Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliweka rekodi katika mbio za barabara za World Athletics Gold Label siku ya hapo jana Jumapili.


Kiplimo ni bingwa mara mbili wa dunia wa mbio za nyika ambaye alishikilia rekodi ya nusu-marathon kutoka 2021 hadi 2024. Alitwaa tena kwa kupunguza sekunde 48 kutoka kwa rekodi ya awali ya dakika 57 na sekunde 30, iliyowekwa na Yomif Kejelcha wa Ethiopia huko Valencia mwezi Oktoba mwaka jana.


Akikimbia katika mazingira bora ya hali ya hewa ya nyuzi joto 13 Selsiasi (13 c) bila upepo. "Nimefurahishwa sana na nilichofanya leo," alisema Kiplimo, ambaye alianza Olimpiki katika mbio za mita 5,000 huko Rio de Janeiro alipokuwa na umri wa miaka 15 pekee.

Commenti


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page