Mkuu wa Maudhui wa Clouds Media Group Sebastian Maganga leo kupitia Power Breakfast ya Clouds FM ameutaja urithi wa Marehemu Gadner G. Habash kwenye kipindi chake cha Jahazi alichokua akikifanya kwa miaka mingi kabla ya kufariki mwezi April 2024.
![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_3aa5065c8e114f87b06914c550ec6133~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_3aa5065c8e114f87b06914c550ec6133~mv2.jpg)
Urithi huo ni Watangazaji wataoliendesha JAHAZI ambapo amewataja kuwa ni Mwenyeji George Bantu, Hamisi Mandi (BDozen), Adam Mchomvu na DJ D Ommy huku Watayarishaji (Producers) wakiwa ni Musa Memba na Big Chawa.
Ikumbukwe kuwa kwa miaka mingi B Dozen na Mchomvu walikuwa wakitangaza kipindi cha mchana cha burudani Double XXL wakiwa na Kennedy The Remedy, Meena Ally pamoja na John Jackson.
Comments