top of page

JAMAA ALIYEZONGWA NA MADENI ABAHATIKA KUPATA ALMASI YA THAMANI YA TSH MILIONI 255



Kutoka India Maisha ya mfanyakazi mmoja yamebadilika ghafla baada ya kupata almasi kubwa katika mgodi wa Madhya Pradesh uliopo jimbo la kati la nchi hiyo.



Almasi hiyo ya karati 19.22 inatarajiwa kuuzwa kwa dola 95,570 za kimarekani sawa na zaidi ya Tsh Milioni 255 katika mnada wa serikali.



Raju Gound amekuwa akikodisha migodi katika jiji la Panna kwa zaidi ya miaka 10 kwa matumaini ya kupata almasi.



Amesema atatumia pesa hizo kujengea familia yake nyumba nzuri na kulipia masomo ya watoto wake. Lakini kwanza, anataka kulipa deni lake la rupee 500,000 sawa na Tsh Milioni 16.



Panna hukodisha migodi ya bei nafuu kwa watu binafsi, familia na makundi ya ushirika ambao hutafuta almasi kwa kutumia zana na vifaa vya kawaida.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page