Na VENANCE JOHN
Muigizaji na muongozaji filamu Bw. John Krasinski leo Jumatano ametajwa kuwa mtu anayevutia zaidi aliye hai katika jarida la People, kwa mwaka 2024, akichukua nafasi kutoka kwa mwigizaji Patrick Dempsey. Krasinski, mwenye miaka 45, amesema kuwa kati ya fursa zote alizpowahi kupata kama mwigizaji, ni kuwa mwanafamilia halisi wa maisha na kwamba hiyo ni thawabu zaidi.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_26c6f6a953714ea68ea45dc89920b240~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_26c6f6a953714ea68ea45dc89920b240~mv2.jpeg)
Krasinski ni mume na baba ambaye anaishi Brooklyn na mke wake mwigizaji Emily Blunt kwa miaka 14 , mwenye miaka 41, na binti zao Hazel wa miaka 10, na Violet wa miaka 8. "Ni jambo zuri sana ambapo unapoolewa na mtu, unajifunza mara kwa mara na kubadilika na kubadilika," mke wake na kuongeza "Na nina bahati sana kupitia hayo yote pamoja naye".
Hivi majuzi, Krasinski ameelekeza vichekesho "IF" na drama "A Quiet Place" na "A Quiet Place Part II," zote zikimshirikisha Blunt katika jukumu kuu. Baada ya kutangazwa hivyo alitania "Nadhani itanifanya nifanye kazi zaidi za nyumbani," akimaanisha wanawake wengi watamtamani ikiwa ataonekana mara kwa mara.
Comentários