Na VENANCE JOHN
Adam Britton ambaye ni mtaalam wa mamba nchini Uingereza amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela nchini Australia, baada ya kukiri kuwadhulumu mbwa kadhaa kingono.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_b13e81de57c841aa93033cd9a7ad5877~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_b13e81de57c841aa93033cd9a7ad5877~mv2.jpg)
Mwanaume huyo ni mtaalamu wa elimu ya wanyama ambaye amewahi kufanya kazi na shirika la utangazaji la Uingereza BBC na filamu za National Geographic, alikiri mashtaka 56 yanayohusiana na unyama na ukatili wa wanyama. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 53 alijirekodi akiwatesa wanyama hao hadi karibu wote wakafa, na kisha kuzichapisha video hizo mtandaoni kwa majina bandia.
Vitendo vyake vya unyanyasaji havikutambuliwa kwa miaka mingi. Britton alikamatwa mwezi, Aprili 2022 baada ya upekuzi kijijini Darwin, ambapo katika upekuzi huo pia viligundulika vifaa vya unyanyasaji wa watoto kwenye kompyuta yake ndogo.
Katika hukumu ya mahakama, Adam, amepigwa marufuku kumiliki mnyama yoyote katika maisha yake yote. Wakili wa Bw. Britton amesema kosa la mteja wake lilitokana na ugonjwa usio wa kawaida unaosababisha mvuto wa kimapenzi usio wa kawaida.
Comments